IQNA

Hali ya Waislamu India

Misikiti karibu na New Delhi yafungwa kufuatia hujuma ya Wahindu wenye msimamo mkali

21:02 - August 06, 2023
Habari ID: 3477390
New Delhi (IQNA) - Misikiti mingi katika kitovu muhimu cha biashara nje kidogo ya mji mkuu wa India, New Delhi ilifungwa kwa sala ya Ijumaa baada ya kifo cha watu sita wakati Wahindu wenye itikadi kali waliposhambulia misikiti na mali za Waislamu.

Polisi walitumwa kwa wingi nje ya misikiti kadhaa huko Gurugram, kitongoji cha New Delhi na kituo kikuu cha biashara ambapo Nokia, Samsung na mashirika mengine ya kimataifa yana makao yao makuu ya India.

Hali ya wasiwasi imekuwa kubwa katika eneo hilo tangu Jumanne wakati kundi la watu waliokuwa na silaha liliposhambulia msikiti mmoja huko Gurugram, na kumuua kasisi mmoja, huku maduka kadhaa na mikahawa midogo ikiharibiwa au kuchomwa moto na makundi ya watu waliokuwa wakiimba nyimbo za kidini za Kihindu.

Hakuna visa vikubwa vya vurugu vilivyoripotiwa tangu Jumanne usiku.

Baadhi ya misikiti huko Gurugram iliruhusu vikundi vidogo kukusanyika kwa ajili ya Sala ya Ijumaa – ambayo ni Sala muhimu zaidi ya wiki kwa Waislamu.

Lakini nyumba tano kuu za ibada za Waislamu katika jiji hilo zilifungwa, huku milango yake ikiwa na vizuizi vikali na polisi.

Maafisa walisema hakuna amri kutoka kwa mamlaka ya kufunga misikiti na kwamba viongozi wa Waislamu wa eneo hilo wametoa wito kwa waumini kusali nyumbani kwa sababu ya mvutano huo.

"Polisi wanahakikisha tu kwamba mipangilio ya usalama ni sawa," afisa mkuu wa polisi Varun Kumar Dahiya aliwaambia waandishi wa habari.

Takriban Waislamu 500,000 wanaishi Gurugram, na eneo hilo limekuwa kitovu cha mzozo wa muda mrefu kuhusu upatikanaji wa ibada.

Tangu Waziri Mkuu Narendra Modi aingie madarakani mwaka wa 2014, India imeshuhudia milipuko mingi ya ghasia kati ya Wahindu walio wengi na Waislamu wake walio wachache India ambao idadi yao ni zaidi ya milioni 200.

Wakosoaji wanakishutumu chama tawala cha utaifwa wa Kihindu,  Bharatiya Janata kwa kuwatenga jamii ya Waislamu tangu kuingia mamlakani.

Machafuko ya kidini huko New Delhi yalisababisha vifo vya watu 53 mnamo 2020.

Na angalau 1,000 waliuawa katika 2002 wakati wa vurugu huko Gujarat, ambapo Modi alikuwa akihudumu kama waziri mkuu wakati huo. Wengi wa wahasiriwa walikuwa Waislamu.

3484642

Habari zinazohusiana
Kishikizo: india waislamu bjp wahindu
captcha