IQNA

Jinai za Israel

Walowezi wa Kizayuni wenye misimamo mikali wauhujumu msikiti mtakatifu wa al-Aqsa

11:26 - August 14, 2023
Habari ID: 3477435
Al-AQSA (IQNA)- Kwa mara nyingine tena walowezi wa Kizayuni wenye misimamo mikali tena wameuvamia na kuuvunjia heshima msikiti wa al-Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israen huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Ripoti zinasema, walowezi wengi wa Kizayuni wenye misimamo mikali jana walivamia msikiti wa al-Aqsa kibla cha kwanza cha Waislamu na kufanya vitendo vya kichochezi huku wakiwa wanapatiwa ulinzi na vikosi vya usalama vya utawala haramu wa Israel.

Msikiti wa al-Aqsa unajulikana kuwa nembo kuu ya utambulisho wa Kiislamu na Kipalestina wa eneo takatifu la Quds na utawala wa Israel unajaribu kuharibu utambulisho huo, lakini kusimama imara na kuwa macho wananchi wa Palestina kumeufedhehesha utawala huo wa Kizayuni na kupelekea njama zake kushindwa.

Hii si mara ya kwanza kwa walowezi wa Kizayuni wenye misimamo mikali kuvamia msikiti wa al-Aqsa wakisaidiwa na wanajeshi wa utawala haramu wa Israel wanaotenda jinai kila uchao dhidi ya ya Wapalestina.

Vitendo vya hujuma za walowezi wa Kizayuni dhidi ya msikiti wa al-Aqsa vimekithiri zaidi baada ya kuingia madarakani serikali yenye misimamo mikali ya Benjamin Netanyahu ambayo imekuwa ikionyesha chuki za wazi wazi dhidi ya Wapalestina na maeneo yao matakatifu.

Vitendo vya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu huko Palestina vinafanyika katika hali ambayo, viongozi wa nchi za Kiarabu na jamii ya kimataifa wameendelea kunyamaza kimya na kutochukua hatua zozote za maana za kukabiliana na vitendo hivyo vinavyokinzana na utu na ubinadamu.

3484760

Habari zinazohusiana
captcha