IQNA

Jinai za Israel

Israel yaendelea kuua watoto wadogo Palestina

17:09 - November 30, 2023
Habari ID: 3477969
UKINGO WA MAGHARIBI (IQNA)- Watoto wawili wa Kipalestina wameuawa shahidi kwa kupigwa risasi na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika mji wa Jenin, kaskazini ya eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Wizara ya Afya ya Palestina imewatambua watoto hao waliouawa shahidi jana Jumatano katika uvamizi wa wanajeshi makatili wa Israel katika eneo hilo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu kuwa ni Adam Samer al-Ghoul (8) na Basil Suleiman Abu al-Wafa (15).

Shirika la habari la Palestina la Wafa limeripoti kuwa, wanajeshi wa Kizayuni mbali na kutekeleza mauaji hayo ya kinyama, lakini pia wameharibu nyumba kadhaa na miundimbinu katika eneo hhilo, na vile vile wameshambulia nyumba moja kwa kuipiga bomu kwa kutumia droni.

Kwa mujibu wa kanali ya televisheni ya al-Mayadeen ya Lebanon, askari wa utawala ghasibu wa Israel wamewatia mbaroni familia nyingi katika mji wa Jenin katika uvamizi wake huo.

Haya yanajiri siku chache baada ya vijana wanne wa Kipalestina kuuawa shahidi kwa kupigwa risasi na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika mji huo wa Jenin, Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Wahanga wa jinai hizo za Israel Ukingo wa Magharibi ni Ammar Muhammad Abu al-Wafa (21), Ahmed Abu al-Hija (20), Muhammad Mahmoud Fraihat (27) na Mahmoud Khaled Abu al-Hija (17).

Gazeti la Kizayuni la Yediot Aharonot limezinukuu duru za kijeshi zikisema kwamba, makadirio ya jeshi la Kizayuni yanaonyesha kuwa, wapiganaji wa muqawama mjini Jenin wanajaribu kurejesha nguvu na uwezo wao wa kijeshi baada ya operesheni za hivi karibuni na wamejikita zaidi kwenye miundombinu na kutengeneza mabomu ya mkono.

Hayo yanajiri wakati ambao tokea Oktoba 7 utawala haramu wa Israel umeua watoto 6000 katika Ukanda wa Gaza wakiwa miongoni mwa watu 15000 waliouawa katika mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala huo dhidi ya raia wa eneo hilo.

Wakati huo huo, Rais wa Marekani lazima aushutumu utawala wa Israel kwa mauaji yake ya watoto wawili wa Kipalestina , kundi la utetezi la Waislamu wa Marekani limesisitiza.
Nihad Awad, mkurugenzi mtendaji wa Baraza la Uhusiano wa Marekani na Kiislamu, alimtaka Rais wa Marekani Joe Biden kulaani mauaji hayo.

Biden "anapaswa kulaani mauaji ya watoto wa Kipalestina kwa njia sawa na ambayo analaani ghasia zinazolenga wengine," alisema katika taarifa.

"Viongozi wa taifa letu lazima hatimaye watambue kwamba Wapalestina ni binadamu ambao wana haki, ikiwa ni pamoja na haki ya kuishi," aliongeza.

3486228

 

Habari zinazohusiana
Kishikizo: watoto palestina gaza cair
captcha