IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Makataa ya kujiandikisha kwa Mashindano ya Qur'ani ya Bint Maktoum ya UAE yatangazwa

16:35 - December 06, 2023
Habari ID: 3477996
DUBAI (IQNA) - Waandalizi wa toleo la 24 la Mashindano ya Qur'ani Tukufu ya Sheikha Hind Bint Maktoum katika Umoja wa Falme za Kiarabu walitangaza Desemba 13 kama tarehe ya mwisho ya usajili.

Tuzo la Kimataifa la Qur'ani Tukufu la Dubai (DIHQA), taasisi ambayo inaandaa mashindano hayo,  lilisema watu wanaopendezwa wanaweza kutuma maombi yao kwa vituo vya kuhifadhi Qur'ani vilivyoidhinishwa hadi Desemba 13.

Mashindano hayo yana kategoria sita: kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu, kuhifadhi Juzuu 20 (sehemu), kuhifadhi Juzuu 10, kuhifadhi Juzuu 5 (washiriki kategoria hii ni raia wa UAE tu), kuhifadhi Juzuu 5 (kwa wakaazi chini ya miaka 10), na kuhifadhi Juzuu 3 (kwa raia raia wa UAE walio chini ya miaka 10).

Ili kushiriki katika shindano hilo, watu wasio raia lazima wawe na umri wa chini ya miaka 25 na wawe na kibali halali cha kuishi katika Umoja wa Falme za Kiarabu. Wakazi wa nchi za Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi pia wanastahili kushiriki ikiwa wana ukaaji wa kudumu katika UAE.

Washiriki lazima wasiwe washindi katika mashindano yaliyopita ya Tuzo ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Dubai au Shindano la Kimataifa la Qur'ani Tukufu la Sheikha Fatima Bint Mubarak, na lazima wasiwe wameshiriki katika kategoria sawa au kategoria ya juu zaidi katika mashindano yaliyotangulia. Kila mshiriki anaweza tu kushiriki katika aina moja ya shindano.

Ibrahim Mohammed Bu Melha, na mshauri wa mtawala wa Dubai kwa masuala ya kitamaduni na kibinadamu na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tuzo hiyo, alisisitiza umuhimu wa Mashindano ya Qur'ani Tukufu ya Sheikha Hind Bint Maktoum.

Mashindano hayo ni tawi muhimu la mashindano ya Qur'ani yaliyoandaliwa na Tuzo ya Qur'ani Tukufu ya Dubai kwa mwaka mzima, alisema na kuongeza kuwa mashindano hayo yanawatambua na kuwaunga mkono wale ambao wamehifadhi Qur'ani miongoni mwa raia na wakazi wa UAE, wanaume na wanawake, na inalenga kuhimiza na kuboresha usomaji na uelewa wao wa mafundisho yake.

Mashindano hayo yatafanyika kuanzia Januari 6 hadi Januari 13, 2024, katika makao makuu ya tuzo katika eneo la Al Mamzar kwa wanaume na katika Jumuiya ya Wanawake ya Al Nahda huko Dubai kwa wanawake. Sherehe ya kufunga na kutunuku washindi itafanyika Januari 16 na 17 kwa wanaume na wanawake mtawalia.

3486314

Habari zinazohusiana
Kishikizo: dihqa qurani tukufu
captcha