IQNA

Harakati za Qur'ani

Casablanca, Morocco kuandaa Tamasha la Kimataifa la Tajweed

17:42 - January 08, 2024
Habari ID: 3478167
IQNA – Duru ya 9 la Tamasha la Kimataifa la Usomaji Qur'ani Tukufu Kwa Tajweed litafanyika Casablanca, Morocco, baadaye mwezi huu.

 

Tamasha hilio lmepangwa Januari 24-27, na itajumuisha mashindano ya usomaji wa Qur'ani Tukufu kwa kuzingatia sheria za Tajweed.

Takriban wasomaji 400 wa Qur'ani kutoka Morocco na baadhi ya nchi nyingine wanatarajiwa katika hafla hiyo ya Qur'ani.

Watashindana katika vikundi viwili vya umri wa watoto na watu wazima katika sehemu mbili, moja kwa wanaume na moja kwa wanawake.

Msomi wa Qur'ani Sheikh Mohammed al-Torabi pia atatunukiwa wakati wa tamasha hilo ambalo huandaliwa kila mwaka na Jumuiya ya Mawasiliano na Maendeleo ya Jamii.

Katika muktadha wa usomaji wa Qur'ani Tukuf, Tajweed ni sheria za matamshi sahihi ya herufi na sifa zote husika kwa njia mbali mbali za kijadi za usomaji.

Morocco ni kitovu cha shughuli za Qur'ani Kaskazini na Magharibi mwa Afrika. Inashikilia matukio na programu mbalimbali za Qur'ani katika ngazi za ndani, kitaifa na kimataifa.

Nchi hiyo ya Kiarabu pia ni kituo cha uchapishaji Misahafu (Nakala za Qur'ani Tukufu) katika mtindo wa Warsh kwa mujibu wa riyawa ya Nafi, ambayo hutumika sana katika eneo hilo.

3486726

Habari zinazohusiana
Kishikizo: morocco qurani tukufu
captcha