IQNA

Ustamaduni wa Kiislamu

Shule za Jadi za Qur'ani Tukufu kuhuishwa nchini Morocco

17:26 - January 16, 2024
Habari ID: 3478202
IQNA - Watu katika mikoa ya kusini mwa Morocco wamekuwa wakirejea tena katika Maktab (shule za jadi za Qur'ani).

Huku migomo ya walimu ikikatiza shughuli za shule za msingi katika mikoa hii, hasa katika jiji la Laayoune, watu sasa wanapeleka watoto wao katika shule za jadi za Qur'ani Tukufu ambazo zinajulikana kama Maktab ili kuendelea na masomo.

Shule hizo sio tu hufunza kusoma Qur'ani Tukufu na sheria zake, lakini pia mafundisho ya Kiislamu na ustadi wa lugha ya Kiarabu, familia zilisema, kulingana na tovuti ya Sawt al-Idalah.

Watoto wanaokwenda Maktab pia huhifadhi Qur'ani Tukufu, ambayo huwasaidia kujifunza vyema na kuweza pia kuhifadhi masomo yao mengine, wanasema.

Maafisa katika jiji hilo wanasema Maktab inatoa fursa kwa watoto kutodhurika na kufungwa kwa shule na wazazi wanaweza kutumia fursa hii.

Wanafunzi wanaoenda Maktab wanaielezea kama uzoefu mpya na njia nzuri ya kuboresha ujuzi wao.

Wanasema ujuzi wanaojifunza katika Maktab unawasaidia kuboresha masomo yao katika shule za kawaida.

Shule za jadi za Qur'ani Tukufu kwa karne nyingi zimetoa elimu ya Qur'ani kwa watoto nchini Morocco.

Katika miaka ya hivi karibuni, serikali, hasa kupitia wizara ya wakfu, imezindua mipango ya kufufua Maktab. Katika eneo la wazungumzao Kiswahili Afrika Mashariki Maktaba kama hizo za Morocco hujulikana kama Madrassah na Duksi katika maeneo ya wanaozungumza Kisomali.

Morocco (Moroko) ni nchi ya Kiarabu ya Kaskazini mwa Afrika inayopakana na Bahari ya Atlantiki na Bahari ya Mediterania. Uislamu ndiyo dini kuu nchini Morocco, huku asilimia 99 hivi ya watu ni Waislamu.

3486830

Kishikizo: morocco qurani tukufu
captcha