IQNA

Vijana katika Ibada

Mamia ya vijana wa Kitanzania washiriki Itikafu

20:15 - January 27, 2024
Habari ID: 3478262
IQNA - Misikiti katika miji tofauti ya Tanzania, ikiwa ni pamoja na Dar es Salaam, Tanga, Kigoma na Moshi iliandaa matambiko ya Itikaf wiki hii.

Mamia ya vijana wenye shauku walishiriki katika ibada hiyo ya kukesha msikitini  iliyofanyika siku za 13, 14 na 15 ya mwezi wa Hijria Qamara wa Rajab (Januari 25-27).

Shughuli hiyo ilifanyika katika misikiti ya Al-Ghadir, Imam Ali (AS), Hujjat al-Asr na misikiti mingine kwa msaada wa jumuiya za kidini na taasisi pamoja na wahisani wa madhehebu ya Shia.

Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Tanzania Mohsen Maarefi alikutana na wale wanaoshiriki ibada katika Msikiti wa al-Ghadir baada ya sala ya Ijumaa jana.

Aliitaja Itikaf kuwa ni fursa ya kutafakari na kujiendeleza kwa wale wanaotafuta kuishi maisha ya kiroho.

Ameongeza kuwa Itikafu ni ibada inayotoa fursa kwa ibada nyengine nyingi kama vile swala, saumu, dua n.k na ndio maana thawabu zinazolingana na zile  za Hijja na Umra huwafikia wanaoshiriki katika itikafu ya siku hizo tatu.

Afisa huyo wa utamaduni wa Iran pia aliwazawadia washiriki katika Itikaf nakala za kitabu cha sheria za Swalah na Wudhu (udhu) kwa lugha ya Kiswahili.

Itikafu ni Sunna ya Mtume Muhammad (SAW) na Ahul Bayt wake, na inachukuliwa kuwa ni ibada yenye thawabu nyingi katika Uislamu.

Ni mazoezi ya kiroho katika Uislamu ambayo yanahusisha kukaa msikitini kwa idadi fulani ya siku, kufunga, na kumwomba Mungu.

Hundreds of Tanzanian Youths Take Part in Itikaf

Hundreds of Tanzanian Youths Take Part in Itikaf

3486968

captcha