IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Ireland: Kiongozi wa Waislamu wa Dublin ashambuliwa kwa 'Uhalifu wa Chuki'

20:23 - February 16, 2024
Habari ID: 3478361
IQNA - Kiongozi mkuu wa Kiislamu mjini Dublin nchini Ireland alivamiwa na watu wawili katika kile alichokitaja kuwa "uhalifu wa makusudi wa chuki" Alhamisi usiku.

Shaykh Umar Al-Qadri, mwenyekiti wa Baraza la Waislamu wa Ireland, alisema alishambuliwa na watu aliokuwa amepanga kukutana nao, RTE iliripoti Ijumaa.

"Kitu ninachokumbuka ni kujisikia kuchanganyikiwa katika gari langu, nikiwa nimezungukwa na majirani wa Kiayalandi wa eneo niliokuwa nikitembelea, wakati gari la wagonjwa lilipofika," aliandika kwenye X, na kuongeza, "Nilijeruhiwa na kupoteza fahamu, lakini  simu yangu ya rununu bado nilikuwa nayo, na niliitumia kuwasiliana na marafiki zangu waliofika ndani ya dakika 15. Walinipeleka hospitalini ambako nililala usiku kucha."

Alipelekwa hospitali ambako alilala usiku kucha. Alisema alivimba usoni na kuharibika meno, lakini hakuna jeraha la ubongo wala kuvunjika taya.

Alitoa shukrani zake kwa majirani waliomsaidia na kusema "anaendelea vyema". Pia alisema waliomshambulia hawakumuibia, bali walikusudia kumdhuru. "Lilikuwa shambulio lililopangwa kabla na uhalifu wa chuki wa makusudi," aliandika.

Polisi walithibitisha kwamba wanachunguza wizi na shambulio lililotokea Tallaght.

Al-Qadri ndiye mwanzilishi wa Irish Muslim Peace and Integration na mkuu wa Kituo cha Elimu na Utamaduni cha Kiislamu nchini Ireland. Amekuwa akiishi Ireland kwa miaka.

3487212/

captcha