IQNA

Harakati za Qur'ani

Taasisi Iran yakamilisha tafsiri ya Qur'ani kwa Kiswidi ili 'Kupambana na Ujinga'

23:06 - April 06, 2024
Habari ID: 3478639
IQNA - Taasisi moja ya Kiislamu nchini  Iran imetangaza kuwa imekamilisha tafsiri ya Kiswidi ya Qur'ani Tukufu katika hatua ya "kupambana na ujahilia" au ujingakufuatia matukio kadhaa ya kuvunjiwa heshima Qur'ani nchini humo mwaka jana.

Taasisi Iran yakamilisha tafsiri ya Qur'ani kwa Kiswidi ili 'Kupambana na Ujinga'

IQNA - Taasisi moja ya Kiislamu nchini  Iran imetangaza kuwa imekamilisha tafsiri ya Kiswidi ya Qur'ani Tukufu katika hatua ya "kupambana na ujahilia" au ujingakufuatia matukio kadhaa ya kuvunjiwa heshima Qur'ani nchini humo mwaka jana.

"Mwaka jana, watu wajinga walichoma nakala za Qur’ani Tukufu mara kadhaa. Kwa kutafsiri Qur’ani Tukufu katika lugha ya Kiswidi, tunalenga kuwaelimisha watu wa Uswidi (Sweden) kuhusu ukweli uliopo katika Qur'ani," Hujjat ul Islam Mohammad Naqdi, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya ya Tarjuman Wahy yenye makao yake Qom, aliiambia IQNA.

Alikuwa akirejelea msururu wa matukio yanayofanywa na watu wenye itikadi kali dhidi ya Uislamu nchini Uswidi ambapo walivunjia heshima nakala za Qur'ani Tukufu. Matukio hayo yalizua malalamiko mengi kutoka kwa Waislamu kote ulimwenguni ambao waliilaumu serikali ya Uswidi kwa kuruhusu vitendo vya kuvunjia heshima Qur’ani Tukufu kwa kisingizio cha kile kinachodaiwa kuwa ni  uhuru wa kujieleza.

"Tafsiri hii ya Kiswidi ni hatua kuelekea kupambana na ujinga," Naqdi aliongeza.

Kwingineko katika mazungumzo hayo, alibainisha kuwa Taasisi ya Utamaduni ya Tarjoman-e Vahy imejitolea kutafsiri Quran katika lugha hai za ulimwengu. "Dhamira hii inatokana na hamu ya mamilioni ya watu kuelewa dhana za Qur'ani katika lugha zao za asili."

Kwa muda wa miaka 20 iliyopita, taasisi hiyo imekuwa nyumbani kwa maprofesa na wafasiri mashuhuri waliobobea katika tafsiri za Qur'ani, alisema.

"Tumefanikiwa kutafsiri Quran katika lugha 15 hai, zikiwemo Kiingereza, Kifaransa, Kihispania, Azeri, Kituruki, Kiurdu, Kirusi, Kichina, Kijapani, Kigeorgia, Kituruki, Kituruki cha Iraqi, Kipashto na Kinyarwanda ," Naqdi alisema na kuongeza kuwa tafsiri zimechapishwa katika nchi mbalimbali, zikiwemo Marekani, Uingereza, Uhispania, Azabajani, Uturuki, India, Uchina, Japan, Urusi, na katika nchi kadhaa  Afrika.

"Katika juhudi zetu za kutafsiri, tulizipa kipaumbele lugha zinazozungumzwa zaidi ulimwenguni ili kuongeza ufikiaji wetu," alisisitiza. Kwa mfano, Naqdi alisisitiza kwamba, Kihispania kinazungumzwa katika nchi 44, na Kiingereza ni lugha ya pili duniani huku Kichina kinazungumzwa na zaidi ya watu bilioni 1.2.

Nchi kama Saudi Arabia, Misri, Libya, na Iran zinashiriki kikamilifu katika miradi kadhaa ya tafsiri za Qur'ani, alisema.

Akilinganisha tafsiri zilizopo za Quran na Biblia, mwanazuoni huyo alisema juhudi zaidi zinahitajika ili kueneza ujumbe wa Qur'ani. "Kufikia 2017, Biblia ilikuwa imetafsiriwa katika lugha 3,200, na kuifanya iweze kupatikana kwa 98% ya watu duniani kote. Kwa bahati mbaya, idadi ya tafsiri au tarjuma za Qur’ani katika ulimwengu wa Kiislamu hailingani kabisa na ile ya Biblia, ikionyesha eneo tunalohitaji kuboresha."

Pia alibainisha kuwa tafsiri mpya ya Kihindi ya Qur’ani Tukufu iko tayari kuchapishwa mwaka huu.

3487822

Habari zinazohusiana
captcha