IQNA

Kikao cha Tafsiri ya Qur'ani nchini Ghana

15:36 - June 12, 2016
Habari ID: 3470378
Mwanazuoni maarufu wa Kiislamu nchini Ghana anatoa darsa za tafsiri ya Qur'ani katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, darsa za msomi hiyo wa madhehebu ya Shia Sheikh Abdul Mumin Alim zinafanyika katika mji wa Tamale kaskazini mwa Ghana. Darsa hizo zinatazamiwa kuendelea hadi mwisho wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani na pia zinarushwa hewani na idhaa moja ya eneo hilo.

Idadi ya Waislamu nchini Ghana inakadiriwa kuwa takribani milioni tatu au asilimia 16 ya watu wote milioni 20 wa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika. Waislamu nchini Ghana wanaishi vizuri na wafuasi wa dini nyinginezo na haki zao zinazingatiwa.

Hivi karibuni pia serikali ya Ghana imewajengea polisi nchini humo msikiti wao maalumu kwa ajili ya kufanya ibada na kujifunza Kiislamu.

Mwezi Machi mwaka jana, Rais John Mahama wa Ghana amesema wanawake Waislamu nchini humo wana haki ya kuvaa vazi la Hijabu.

Rais wa Ghana alisema anafungamana na utekelezwaji wa kifungu cha 21 katika katiba ya nchi ambacho kinawapa raia uhuru wa kuabudu.
'Ni kinyume cha katiba kuwalazimu wanafunzi Waislamu kuenda kanisani au wanafunzi Wakristo kulazimishwa kuenda msikitini', amesema Rais wa Ghana. Aidha amesema, 'Si sahihi kuwazuia wanawake Waislamu kuvaa Hijabu au kuwazuia watawa wa kike kikatoliki kuvaa vazi lao.'

3506130
Kishikizo: ghana iqna
captcha