IQNA

Wawakilishi wa nchi 31 kushiriki fainali ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Malaysia

17:08 - October 08, 2022
Habari ID: 3475896
TEHRAN (IQNA) - Kwa mujibu wa maafisa, washiriki 41 kutoka nchi 31 wamepangwa kushiriki katika duru ya mwisho ya toleo la 62 la Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Malaysia.

Duru ya mwisho ya mashindano hayo ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani inatazamiwa kufanyika kuanzia Oktoba 19 hadi 24 katika Kituo cha Mikutano cha Kuala Lumpur (KLCC). Duru ya awali ilifanyika karibu Julai.

Kwa mujibu wa Datuk Haji Idris bin Ahmad, Waziri katika Idara ya Waziri Mkuu (Masuala ya Kidini), nchi ambazo wawakilishi wake wametinga fainali ni pamoja na Algeria, Jordan, Uingereza, Canada, Afghanistan na Ubelgiji.

Mashindano hayo yaliahirishwa kwa miaka miwili na nusu kwa sababu ya wasiwasi juu ya janga la COVID-19.

Masoud Nouri ni mwakilishi wa Iran katika shindano hilo. Idara ya Maendeleo ya Kiislamu Malaysia, inayojulikana zaidi kama JAKIM  huandaa mashindano hayo kila mwaka.

4090276

captcha