IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Ali Reza Bijani kuiwakilisha Iran katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Malaysia 2023

19:25 - May 17, 2023
Habari ID: 3477013
TEHRAN (IQNA) - Ali Reza Bijani ataiwakilisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Mashindano ya 63 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Malaysia.

Hayo yamedokezwa na Hamid Majidimehr, Mkuu wa Kituo cha Masuala ya Qur'ani cha Shirika la Wakfua na Misaada ambaye amebaini kuwa qari huyo alichaguliwa kuwa mwakilishi wa nchi katika mashindano hayo wakati wa kikao cha hivi karibuni kati ya maafisa wa shirika  na Kamati ya Kuwaalika na Kuwatuma Maqarii.

Amebainisha kuwa uteuzi huo ulifanywa baada  kuwatathmini wale wote waliopata nafasi za juu katika mashindano ya kitaifa ya Qur'ani ya Iran.

Majidimehr ameongeza kuwa, uamuzi huo umetolewa baada ya kuzingatia masharti na kanuni za tukio la kila mwaka la kimataifa la Qur'ani nchini Malaysia.

Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Malaysia, yanayojulikana rasmi kama Mkutano wa Kimataifa wa Kuhifadhi na Kuhifadhi Qur'ani ya Malaysia (MTHQA), huandaliwa kila mwaka katika mji mkuu wa nchi hiyo wa Kuala Lumpur.

Ali Reza Bijani to Represent Iran at Malaysia Int’l Quran Contest 2023

Bijani alizaliwa mwaka 1994 katika Mkoa wa Razavi Khorasan, kaskazini-mashariki mwa Iran. Pia ni mwanafunzi wa Seminari ya Kiislamu huko Mashhad.

Alishika nafasi ya kwanza katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Bangladesh mwaka 2021.

Pia alikuwa ametwaa tuzo ya juu zaidi katika mashindano ya kitaifa ya Qur'ani ya Iran mwaka 2019.

4141180

captcha