IQNA

WHO: Hali ya kiafya Yemen ni mbaya sana

15:55 - July 16, 2015
Habari ID: 3328804
Shirika la Afya Duniani WHO limeonya kuhusu hali mbaya ya kibinadmau nchini Yemen na kusema na kusema mkoa wa Aden unakabiliwa na hali maafa ya kiafya.

Mwakilishi wa WHO nchini Yemen Ahmed Shadoul amesema Jumanne kuwa, "hali ya kibinadamu na kiafya Yemen ni mbaya sana na hali hiyo inazidi kuzorota."
Wakati huo huo Mashirika ya kibinadamu nchini Yemen yametoa wito wa ufadhili na kuwezeshwa kuwafikia wahitaji kwa dharura. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Kuratibu masuala ya Kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, OCHA, mashirika hayo yametoa wito kwa pande pinzani katika mzozo wa Yemen kuwalinda raia kulingana na sheria za kimataifa za kibinadamu, pamoja na kuwezesha wahudumu wa kibinadamu kufikisha usaidizi kwa watu wanaouhitaji.
Taarifa imesema, raia wa Yemen wameendelea kuteseka wakati machafuko yakiongezeka bila kuonyesha dalili ya kusitishwa, wiki hii ikiwa imeshuhudia maafa makubwa zaidi tangu mwezi Machi.
Takriban watu milioni 1.3 wamelazimika kuhama makwao kwa sababu za kiusalama, huku wengine wanaohitaji misaada ya kibinadamu, wakiwa ni milioni 21, ambayo ni sawa na asilimia 80 ya idadi nzima ya watu Yemen.
Mahitaji ya kibinadamu yamezidi uwezo wa kutoa usaidizi, huku ombi la ufadhili likiwa limepokea asilimia 15 tu ya dola bilioni 1.6 zinazohitajika hadi mwishoni mwa mwaka huu 2015.
Saudi Arabia ilianza kuishambulia kijeshi Yemen tangu tarehe 26 Machi, na hadi sasa watu zaidi ya 4,600 wameshauawa wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto. Saudia imekiuka mapatano ya usitishwaji vita yaliyokuwa yameanza kutekelezwa Ijumaa iliyopita kupitia upatanishi wa  Umoja wa Mataifa.  Saudia imezidhisha hujuma dhidi ya watu wa Yemen katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.  Aidha Saudi Arabia pia imevurumisha mabaomu katika maeneo ya raia Yemen kama vile mahospitali, shule na hata misikiti.../mh

3328487

captcha