IQNA

Iran kuwa kitovu cha utalii Halali duniani

16:20 - September 02, 2015
Habari ID: 3357519
Makamu wa Rais wa Iran na Mkuu wa Shirika la Utamaduni na Turathi Masoud Soltanifar amesema shirika hilo linapanga kuigezua Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa kitovu cha utalii Halali duniani.

Akizungumza na IQNA, Solfanifar amesema kufuatia kuondolewa vikwazo dhidi ya Iran, serikali sasa imejikita katika kuimarisha sekta ya utalii ili kuandaa mazingira ya Iran kuwa kivutio kikuu cha utalii halali duniani.
Amesema sekta ya utalii Iran imeshuhudia ustawi mkubwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita na kuongeza kuwa, kumekuwepo na ongezeko kubwa la watalii wanaoitembelea Iran kutoka nchi mbali mbali duniani hasa nchi jirani za Kiislamu. Amesema kwa kuzingatia utalii halali na pia ziara katika maeneo matakatifu, Iran inaweza kuwa kivutio kikubwa kwa watalii Waislamu.
Ameongeza kuwa asilimia 50 ya raia wa kigeni wanaotembelea Iran hufika nchini kutembelea haram takatifu za Imam Ridha AS mjini Mashhad na Bibi Maasoumah SA mjini Qum. Soltanifar amesema baina ya Machi 2014 na Machi 2015, watalii milioni 5 wa kigeni walitembelea maeneo ya kidini, kihistoria na kiutamaduni nchini Iran.
Amesema kati ya watalii hao milioni 1.6 walikuwa kutoka Iraq, laki tano kutoka  Saudi Arabia, Kuwait na Bahrain pamoja na nchi zingine za kusini mwa Ghuba ya Uajemi huku laki tatu wakiwa kutoka nchi kama vile India, Pakistan na Afghanistan. Soltanifar amesema pia kuna idadi kubwa ya watalii kutoka nchi za Ulaya na Kusini Mashariki mwa Asia ambao hutembelea vivutio vya kitalii nchini.
Utalii Halali ni istilahi inayotumika kumaanisha utalii unaolenga kuwavutia Waislamu na familia zao. Huu ni utalii ambao huzingatia kanuni na sheria za Kiislamu ambapo, kwa mfano hoteli husika huwa haziuzi pombe na wala majumba ya kamari n.k na wala wanawake na wanaume hawaogelei sehemu moja.Aidha hoteli kama hizo huhakikisha kuwa chakula kinachopikwa huwa ni halali na kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu.../mh

3357196

Kishikizo: utalii iran halali kiislamu
captcha