IQNA

Utalii wa Kiislamu

Malaysia yazindua mpango wa kuvutia Watalii Mwezi wa Ramadhani

16:39 - January 18, 2024
Habari ID: 3478210
IQNA - Mpango umezinduliwa nchini Malaysia ili kuvutia watalii wa ndani na nje katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Wizara ya Utalii, Sanaa, na Utamaduni kupitia wakala wake wa Tourism Malaysia kwa ushirikiano na Kituo cha Utalii wa Kiislamu (ITC), Chama cha Hoteli za Malaysia (MAH), na Chama cha Wamiliki wa Hoteli cha Malaysia (MAHO), ilitangaza uzinduzi wa Mpango wa Uzoefu Wangu wa Ramadhani.

Mpango huu unatoa fursa isiyo na kifani ya kujitumbukiza matukio ya kusisimua ya Mwezi Mtukufu wa  Ramadhani nchini Malaysia.

Mpango huo unalenga kuwapa watalii  uzoefu wa kitamaduni unaochanganya na sekta ya hoteli na migahawa Halal ili kuvutia watalii wa ndani na kimataifa wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Ikiwakilisha juhudi za pamoja, mpango huu unatumia utaalam wa sekta zote husika ili kuratibu orodha pana ya hoteli zinazotoa vifurushi vya malazi vinavyovutia. Vifurushi hivi vilivyoundwa kwa ustadi ni pamoja na Iftar ya ziada kwa watu wawili, kuhakikisha kuwa hoteli zinazoshiriki zina cheti cha kifahari cha "Jiko la Halal" kutoka Idara ya Maendeleo ya Kiislamu Malaysia (JAKIM).

Mpango wa Uzoefu Wangu wa Ramadhani unaonyesha matukio mbali mbali mambo muhimu ikiwa ni pamoja na kuwaalika washiriki kuchunguza soko za Ramadhani, Futari  kwenye misikiti mikubwa, kushiriki katika programu za Iftar zinazoongozwa na serikali/NGO, na kushiriki katika shughuli kama vile kupika vyakula maarufu nchini Malaysia.

Kwa kuzingatia watalii wa ndani na wa kimataifa, programu inalenga kuangazia mvuto wa kutembelea Malaysia wakati wa mwezi huu mtakatifu. Miji  ya  Kuala Lumpur, Putrajaya, na Selangor itaongoza katika kuwapokea watalii katika Mwezi. 

3486848

captcha