IQNA

Kukithiri chuki dhidi ya Waislamu London

11:58 - September 09, 2015
Habari ID: 3360838
Takwimu mpya zinaonyesha kuwa idadi ya jinai zinazosababishwa na chuki dhidi ya Waislamu zimeongezeka nchini Uingereza mwaka uliopita.

Takwimu zilizotolewa na Polisi ya London zinaonyesha kuwa Waislamu katika mji mkuu huo wameshuhudia ongezeko la asilimia 70 ya mashambulizi ya chuki dhidi ya dini Tukufu ya Uislamu katika kipindi cha mwaka mmoja. Jumla ya vitendo vya chuki dhidi ya Waislamu 816 vimesajiliwa katika muda wa miezi 12 hadi kufikia mwezi Julai mwaka huu. Vitendo hivyo vya chuki dhidi ya Waislamu vilikuwa 478 katika muda kama huo kati ya mwaka 2013 na 2014. Msemaji wa Tell MAMA, kundi linalofuatilia mashambulizi hayo ya chuki dhidi ya Waislamu amesema kuwa, walengwa wengi wa hujuma hizo ni wanawake wanaovaa hijabu. Jumuiya za walimu na makundi yanayopinga ubaguzi nchini Uingereza yalitahadharisha juu ya ongezeko la ubaguzi dhidi ya Waislamu mashuleni yakisema kuwa, jambo hilo litaandaa mazingira ya mashaka na hofu miongoni mwa wanafunzi wa Kiislamu. Makundi hayo pia yameikosoa na kuilaumu serikali ya London kwa kushindwa kushughulikia suala hilo.../mh

3360051

captcha