IQNA

Kituo cha Kiislamu cha Uingereza kuadhimisha kuzaliwa Bibi Fatima Zahra (SA)

15:55 - December 31, 2023
Habari ID: 3478123
IQNA - Kituo cha Kiislamu cha Uingereza kitaandaa sherehe kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Bintiye Mtume Muhammad (SAW), Bibi Fatima Zahra (SA).

Sherehe hiyo imepangwa Jumanne, Januari 2, usiku wa kuamkia hafla hiyo ya furaha.

Idadi kadhaa ya maulama na shakhsia wa Kiislamu, wakiwemo Ayid Qassim al-Jalali, Sheikh Mirza Abbas, Basem al-Daraji, Sheikh Mohammad Jafar Salehi na Sheikh Mohammad Bakhtiari watahudhuria programu hiyo.

Kituo hicho kimewaalika Waislamu wote wa madhehebu ya Shia na maashiki wa Ahl-ul-Bayt (AS) kushiriki katika maadhimisho hayo.

Siku ya 20 ya mwezi wa Jumada al-Thani katika kalenda ya mwandamo ya Hijria Qamaria, inayoadhimishwa Jumatano, Januari 3, mwaka huu, ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa binti kipenzi cha Mtume Mtukufu (SAW).

Pia inaadhimishwa kama siku ya wanawake na siku ya mama katika jamii nyingi za Waislamu..

Kituo cha Kiislamu cha Uingereza (ICEL) kilianzishwa mnamo 1998.

Kulingana na tovuti yake, ICEL ni kituo cha kidini na kitamaduni kinachotoa huduma zifuatazo:

- Mwongozo wa kiroho na kimaadili kwa umma wa Kiislamu kwa ujumla;

- Kukidhi mahitaji ya kijamii, kitamaduni, kielimu na burudani ya wanajamii, hasa wanawake na kizazi kipya;

- Kusambaza elimu halisi ya Kiislamu ili kutoa ufahamu bora wa Uislamu kwa watu wa imani nyingine;

- Kuunda mizinga ya Kiislamu ili kufanya mazungumzo juu ya maswala ya kisasa kama vile magonjwa ya milipuko na shida za mazingira;

- Na kuanzisha uhusiano wa karibu na watu wa imani na tamaduni tofauti kutoka kote ulimwenguni.

3486622

Kishikizo: london Bibi Fatima
captcha