IQNA

Meya wa Kwanza Mwislamu achaguliwa London

10:53 - May 07, 2016
Habari ID: 3470297
Sadiq Khan wa chama kikuu cha upinzani cha Leba nchini Uingereza amechaguliwa kuwa Meya wa mji wa London na hivyo kuwa Meya wa kwanza Mwislamu kuuongoza mji huo mkuu.
Aidha ni mara ya kwanza kwa Mwislamu kuchaguliwa kuongoza mji wa nchi ya Umoja wa Ulaya

Sadiq Khan Mwingereza mwenye asili ya Pakistan ambaye alikuwa anagombea nafasi hiyo na wapinzani zaidi ya wawili, amefanikiwa kushinda umeya kwa asilimia 56.8 akifuatiwa kwa karibu na mshindani wake mkuu Tory Zac Goldsmith ambaye amepata asilimia 43.2.

Sadiq Khan mwenye umri wa miaka 45 anakuwa Meya wa kwanza Mwislamu kuiongoza London katika historia ya mji huo. Kuchaguliwa Khan ni pigo kubwa kwa Waziri Mkuu David Cameroon na chama cha wahafidhina au Conservative.

Kwa matokeo hayo Sadiq Khan atachukua kiti cha Umeya wa London akimrithi Boris Johnson Meya mwenye utata mwingi ambaye anaondoka baada ya kuwa meya kwa miaka minane na ambaye amekuwa akiongoza kampeni ya Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya. Kiongozi wa chama cha Leba Jeremy Corbyn amemponga Khana na kusema ushindi wake utapelekea uadilifu kutendeka kwa wote mjini London.

3495421
captcha