IQNA

Mwamko dhidi ya Marekani

Azimio la Maandamano ya Siku ya Taifa ya Kupambana Ubeberu nchini Iran

17:30 - November 04, 2022
Habari ID: 3476032
TEHRAN(IQNA)- Washiriki katika maandamano ya Siku ya Taifa ya Kupambana na Ubeberu inayosadifiana na leo 4 Novemba, wamesisitiza udharura kuwepo mapambano endelevu dhidi ya njama za kuzusha fitna, ghasia na fujo.

Washiriki katika maandamano ya leo ya kupinga ubeberu wa kimataifa ambao walikuwa wakipiga nara za "Mauti kwa Marekani" kuonyesha kuchukizwa kwao na siasa za kiuadui na kibeberu za mfumo wa ubeberu unaoongozwa na serikali ya Washington, wametangaza uungaji mkono wao kwa hatua za kimapinduzi za Bunge, Serikali na Idara ya Mahakama hapa nchini na kusisitiza udharura wa kudumishwa mapambano dhidi ya wanaozusha fitina na ghasia. Vilevile azimio lililotolewa mwishoni mwa maandamano hayo limewataka viongozi wa nchi kutofautisha baina ya watu walioeleza malalamiko yao katika matukio ya hivi karibuni hapa nchini na wale wanaozusha ghasia na fujo, na kutayarisha mazingira ya kisheria ya ukosoaji wa wananchi. 

Azimio la mwisho la maandamano ya leo pia limewaenzi mashahidi waliouawa katika shambulio la kigaidi katika Haram Tukufu ya Hadhrat Ahmad Ibn Musa (AS) huko Shiraz na kusema: Jinai hiyo ya kutisha na kimya cha wanaodai kutetea haki za binadamu ni ushahidi wa kina cha chuki na kielelezo cha uovu wa dhalimu mkubwa, Marekani, na ni alama ya mkono wa adui muwasha moto na vibaka wake wasaliti, majahili na walioghafilika dhidi ya taifa kubwa la Iran ya Kiislamu.

Katika azimio hilo imeelezwa kuwa: Washiriki wa maandamano 13 Aban (4 Novemba) wakiwa na uelewa mzuri kuhusu ubeberu wa kimataifa, wanafahamu vyema kwamba njama za mashirika ya ujasusi ya Marekani, Uingereza na utawala wa Kizayuni na unaoua watoto wa Israel, na kwa msaada wa tawala fasidi za Al-Saud na Uingereza, na hujuma za mtandaoni zisizo na kifani na kwa usaidizi wa watu mashuhuri vibaraka waliopoteza utambulisho wao ambao wamefeli katika ghasia za hivi karibuni, hawataacha kuwaandama vijana wa nchi hii; kwa msingi huo familia, walezi, walimu na wahadhiri walioelimika na maafisa wa masuala ya utamaduni wa nchi wanaombwa kulipa uzito suala la kubainisha ukweli na kuzima njama na mipango ya maadui kwa kudumisha umakini, kuwasiliana na kufanya mazungumza na kizazi kipya.

Washiriki katika maandamano ya Siku ya Taifa ya Kupambana na Ubeberu wa Kimataifa pia wamewashukuru wanafunzi na walimu walioko mstari wa mbele katika hatua ya pili ya Mapinduzi ya Kiislamu, ambao wamesimama imara dhidi ya makundi yanayofanya uchochezi katika vituo vya elimu.

Ikumbukwe kuwa

Miaka 43 iliyopita katika siku hii (Aban 13, 1358, sawa na Novemba 4, 1979), wanachuo wa vyuo vikuu vya Iran waliliteka Pango la Ujasusi la Marekani (Ubalozi) mjini Tehran kulalamikia njama kadhaa wa kadhaa zilizokuwa zikifanywa na Marekani dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Tarehe 13 Aban, sawa na Novemba 4 ni kumbukumbu ya matukio matatu muhimu katika vipindi vitatu nyeti na hasasi vya historia ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Matukio hayo matatu muhimu ya kumbukumbu ni siku aliyobaidishwa na kupelekwa uhamishoni nchini Uturuki Imam Khomeini (MA) tarehe 4 Novemba 1964, siku waliyouliwa wanafunzi na askari wa utawala wa Pahlavi Novemba 4, 1978 na siku ilipofanyika harakati ya kimapinduzi ya kuliteka Pango la Ujasusi la uliokuwa ubalozi wa Marekani mjini Tehran.

Harakati hiyo ya Novemba 4, 1979 ilitekelezwa na wanachuo wafuasi wa njia ya Imam Khomeini (MA), mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Kila moja kati ya matukio hayo matatu ilikuwa hatua muhimu sana katika mchakato wa harakati za taifa la Iran za kupambana na Uistikbari.

4096820

captcha