IQNA

Uchumi na Uislamu

Utalii wa Kiislamu unaweza kuwa na pato la $230 Bilioni kufikia 2028

17:19 - November 13, 2022
Habari ID: 3476082
TEHRAN (IQNA) – Kongamano la utalii wa Kiislamu (Ziyarah) lilifanyika Samarkand, Uzbekistan, ambapo wazungumzaji walisema utalii huo unaweza kupata pato la dola bilioni 230 ifikapo 2028.

Utalii wa Kiislamu pia unaweza kuchukua jukumu muhimu katika ushirikiano wa kiuchumi wa nchi za Kiislamu, walisema.

Walisema hivi sasa idadi ya watu katika ulimwengu wa Kiislamu ni bilioni 2.3, ambayo ni asilimia 27 ya watu wote duniani na hivyo hii ni fursa kubwa kwa shughuli za kiuchumi na utalii.

Kongamano la Utalii wa Kiislamu (Ziyarah) na "Wiki ya Kimataifa ya Utalii ya Ziyarah" ilifanyika Samarkand chini ya usimamizi wa Wizara ya Utalii na Turathi za Utamaduni ya Uzbekistan.

Wazungumzaji walisema kuwa kila mwaka watalii Waislamu milioni 160 hufanya Ziyarah za kidini au safari zingine za kitalii za kimataifa, ambapo idadi yao itaongezeka hadi 230 ifikapo 2028.

Walisema kuwa Uzbekistan kama kitovu cha utamaduni na turathi za Kiislamu inaweza kuwa na jukumu kubwa la kukuza utalii wa Kiislamu, mkutano wa leo wa Ziyarah ni ishara kwamba Uzbekistan inafanya juhudi kubwa katika suala hili.

Wakati huo huo, Naibu Waziri Mkuu wa Uzbekistan na Waziri wa Utalii na Urithi wa Utamaduni Aziz Abduhakimov alisema kuwa mwaka huu serikali yetu iliamua kuandaa "Wiki ya Kimataifa ya Utalii ya Ziyarah" kwa ajili ya kukuza utalii wa Kiislamu.

Katika mwaka huu wa 2022, wajumbe 150 kutoka nchi mbalimbali wameshiriki katika Kongamano hili la Utalii (Ziyarah) la miaka 2022, na watatoa maoni yao kwa ajili ya kukuza utalii wa Kiislamu wakati huu, alisema.

Naibu Waziri Mkuu alisema kuwa huu umetangazwa rasmi kama mwaka wa utalii nchini Uzbekistan na utalii wa Kiislamu una uwezo mkubwa nchini Uzbekistan.

Amesema kuwa, miji ya Samarkand, Bukhara na Khiva ya miji ya Uzbekistan ina madhabahu ya Watakatifu na wanazuoni, na sambamba na hayo, walizaliwa wasomi na wanasayansi wengi wa Kiislamu katika nchi hii, ambao walipata umaarufu wa dunia katika uwanja wao.

Aziz Abduhakimov alisema Kongamano la utalii litakalofanyika Uzbekistan litaongeza ushirikiano wa utalii na nchi zote za Kiislamu duniani.

Alisema kuwa kufanya mkutano huo kutaimarisha ushirikiano wa Uzbekistan na nchi nyingine katika siku zijazo na kukuza utalii wa ndani.

Alisema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa utalii wa Kiislamu nchini Uzbekistan ambao unaweza kutembelewa na watalii kutoka nchi za Kiislamu.

Naibu Waziri Mkuu alisema kuwa Samarkand ndio kitovu cha utalii cha Uzbekistan ambapo kuna fursa kubwa za utalii. Kwa njia hii, "tunatoa vifaa vya kisasa vya utalii na kila aina ya miundombinu mahali hapa, ambayo itakuza utalii wa ndani."

Amesema Samarkand pia ni kitovu cha dunia cha turathi za utamaduni na sayansi ya Kiislamu, ambapo wanasayansi wakubwa na wanasosholojia na wanazuoni mashuhuri duniani walizaliwa.

Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Utalii cha Kiislamu (Wizara ya Utalii, Malaysia), Dk Muhammad Razip Hasan, alisema Uzbekistan ina asili yake na ina uwezo mkubwa katika utalii wa Kiislamu ambao unaweza kuboresha uchumi wa nchi za Kiislamu.

Alisema hivi sasa asilimia 70 ya vijana duniani wako katika nchi za Kiislamu, jambo ambalo linaweza kuwa na nafasi muhimu katika shughuli hizo.

Razip Hasan alisema kuwa utalii ni uti wa mgongo wa uchumi wa kisasa, ambao nchi za Kiislamu zinatakiwa kuufanyia kazi.

Alisema kuwa utalii una nafasi muhimu sana katika uchumi wa Malaysia na serikali yetu inazingatia sana vifaa vyake.

Fazal Bahardeen, mtaalamu wa masuala ya utalii wa Kiislamu na soko la halal na mtafiti amesema kuwa, utalii wa Kiislamu una thamani kubwa katika uchumi wa dunia ambao utafikia dola bilioni 230 katika miaka 6 ijayo.

Alisema kuwa utalii wa Kiislamu una fursa nyingi katika Uzbekistan, Saudi Arabia, Iran, Pakistan na Iraq. Vile vile, katika zama za sasa, kuna uwezekano wa dola trilioni 2.5 katika soko la dunia la bidhaa za chakula za Halal, ambazo nchi za Kiislamu zinaweza kupata faida za kiuchumi.

Alisema iwapo sekta hii itakubaliwa katika ngazi rasmi, ushirikiano wa kiuchumi unaweza pia kutokea katika nchi za Kiislamu.

3481241

captcha