IQNA

Fikra za Kiislamu

Haki za Utajiri kwa mtazamo wa Imam Sajjad AS

18:56 - November 25, 2022
Habari ID: 3476146
TEHRAN (IQNA) – Mitihani kutoka kwa Mwenyezi Mungu inakujakwa njia mbalimbali na utajiri ni njia mojawapo ya kuwatahini wanadamu. Kuna mapendekezo mengi katika Qur’ani Tukufu na maandishi mengine ya Kiislamu kuhusu jinsi ya kupata na kutumia mali.

Imam Sajjad (AS), Imamu wa nne wa Madhehebu ya Shia, ana kitabu kiitwacho, “Risala ya Haki” (Risalat Al-Huquq) ambamo anataja aina mbalimbali za haki.

Sehemu moja ya maandishi hayo  imejikita  kwenye haki ya utajiri:

 “Haki ya mali yenu ni kuwa muichume kwa njia halali na muitumie kwa njia ya haki. Ukiwa na mali haupaswi kujipendelea kuliko wale ambao hawatakusifu. Unatakiwa uitumie mali katika kumtii Mola wako Mlezi wala usiwe bakhili nayo, usije ukajipata katika hali ya majuto huku ukikumbana  matokeo mabaya. Na hakuna nguvu ila kwa Mwenyezi Mungu.

Kwa mujibu wa Imam Sajjad (AS), haki ya mali ni kupatikana kutoka kwa chanzo cha halali na kutumika katika njia ya halali.

Hili ni muhimu sana hivi kwamba kama mtu atasema katika wosia wake kwamba sehemu ya mali yake itumike kwa mayatima, watoto wake hawawezi kutumia pesa hizi kwa mambo mengine hata kama ni mazuri

Pendekezo lingine ni kwamba usikabidhi mali yako kwa mtu ambaye anaweza kutumia utajiri huu kwa njia haramu.

Imam Sajjad AS pia anasema kuna wale ambao wameweza kupata mali lakini wakashindwa kutumia utajiri huo katika njia ya Mwenyezi Mungu. Pengine watoto wao watatumia utajiri huo kwa matendo mema na watajuta kwa nini hawakuifanya wao wenyewe.

Kuna aya mbalimbali za Qur’ani Tukufu zinazosema kuwa na mali ni mtihani na kwamba wanadamu wanapaswa kufahamu jinsi wanavyoipata na kuitumia.

 Makala haya ni sehemu ya  muhadhara uliotolewa na mfasiri maarufu wa Qur’ani Tukufu Mohsen Qara’ati.

captcha