IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Msikiti wa Glasgow watangaza ratiba ya Ramadhani

20:55 - March 03, 2023
Habari ID: 3476649
TEHRAN (IQNA) – Msikiti Mkuu wa Glasgow, Scotland nchini Uingereza umetangaza ratiba ya shughuli za ibada katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu wa 1444 Hijria Qamaria.

Taarifa ya msikiti huo imesema inakadiriwa kuwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani utaanza Machi 23 au 24 kwa kutategemea mwezi mwandamo.

Waislamu  zaidi ya bilioni moja na nusu kote duniani wanajiandaa kwa ajili ya Saumu ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kwa kuzingatgia majira ya machipuo ya mwaka huu,  wakaazi wa Glasgow wanatazamiwa kufunga hadi masaa 15 kwa siku.  

Msikiti Mkuu wa Glasgow umetoa ratiba ya Ramadhani 2023 yenye maelezo kuhusu nyakati za Sala na pia sherehe za siku kuu ya Idul Fitr ambayo huashiria kumalizika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Msikiti Mkuu wa Glasgow unatambuliwa kuwa moja ya misikiti ya kijani zaidi duniani kwa maana kuwa unazingatia utunzaji mazingira katika shughuli zake. Msikiti huo hutumia nishati ya jua kikamilifu.

Kutokana na jitihada hizo, msikiti huo wa Glasgow unatumiwa kama mfano wa kuigwa katika kuhimiza misikiti mingine duniani itumie nishati ya miale ya jua ili kutunza mazingira na kupunguza gharama.  

3482675

captcha