IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Aya za Kila Siku: Ramadhani, Mwezi wa Kuteremshwa Qur'ani Tukufu

13:18 - March 23, 2023
Habari ID: 3476746
TEHRAN (IQNA) – Mwezi uliobarikiwa wa Ramadhani ni wakati Mwenyezi Mungu Mtukufu alipoteremsha Qur’ani Tukufu kwa Mtume Muhammad (SAW) kama mwongozo kwa wanadamu.

Hivi ndivyo tusomavyo katika aya ya 185 ya Surah Al-Baqarah.

Daily Verses: Ramadan Month of Quran Revelation  

Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Basi ataye kuwa mjini katika mwezi huu naafunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru.

captcha