Jana Alkhamisi, kafiri anayeupiga vita Uislamu anayejulikana kwa jina la Salwan Momika aliitovukia adabu tena nakala ya Qur'ani Tukufu mjini Stockholm, kwa ulinzi kamili wa jeshi la polisi la Uswidi
Baraza la Uratibu wa Tablighi ya Kiislamu la Iran limetoa taarifa ya kulaani jinai ya kibaraka huyo wa madola ya Magharibi na kuwataka Waislamu wote duniani na kila mpenda haki kufanya maandamano ya kulaani jinai hiyo.
Taarifa ya baraza hilo imesema, siasa za kueneza chuki dhidi ya Uislamu na kuhatarisha usalama wa dunia kupitia kueneza misimamo mikali na kujeruhi hisia za mabilioni ya watu duniani, haziwadhuru Waislamu peke yao, hivyo kila mwenye fikra huru ana wajibu wa kusimama imara kulaani siasa hizo za kijinai.
Baada ya Sala za Ijumaa zilizosaliwa katika maeneo tofauti ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, wananchi wa Iran leo wamejitokea kwa kwa wingi katika maandamano ya kulaani jinai ya kuvunjiwa tena heshima Qur'ani Tukufu huko Uswidi na kutaka hatua kali zichukuliwe dhidi ya serikali ya Stockholm.
4156799/4156707