IQNA

Uislamu kwa watu wote

Nakala za Qur'ani kwa maandishi ya Braille kwenye Maonyesho ya Vitabu ya Cairo

17:38 - January 28, 2024
Habari ID: 3478267
IQNA - Nakala za Qur'ani Tukufu na vitabu vya Kiislamu katika maandishi ya maandishi ya nukta nundu au kwa lugha ya kiingereza Braille, ni miongoni mwa vitu vilivyoonyeshwa kwenye toleo la 55 la Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Cairo.

Jumuiya ya Mazaya ya Wenye Ulemavu wa Macho imewasilisha vitabu hivyo katika mabanda 4, kulingana na tovuti ya Youm7.

Lengo limetajwa kuwa ni  kuongeza uelewa kwa umma kuhusu shughuli na hatua zinazochukuliwa kwa ajili ya kukuza ufundishaji wa Qur'an na sayansi za kidini kwa wenye ulemavu wa macho.

Vitabu vya Braille viko kwenye mada tofauti kama vile tafsiri za Qur'an, Sira ya Mitume Muhammad  SAW, haki za wanawake na kazi za wanazuoni wa Qur'ani wa Misri.

Braille ni mfumo wa kuandika ambao huwawezesha vipofu na watu wasioona vizuri kusoma na kuandika kwa kugusa.

Ilivumbuliwa na Louis Braille (1809-1852), ambaye alikuwa na ulemavu wa macho na akawa mwalimu wa wenye ulemavu wa macho.

Katika miaka ya hivi karibuni, Qur'ani Tukufu na vitabu vya kidini vimechapishwa katika maandishi ya nukta nundu ili kuwasaidia Waislamu wenye matatizo ya kuona kusoma maandiko kwa urahisi.

Kufundisha Qur'ani Tukufu kwa watu wenye ulemavu wa macho imekuwa ni utamaduni kwa muda mrefu na wengi miongoni mwa maqari maarufu nchini Misri na wahifadhi Qur'ani wamekuwa ni watu ulemavu wa macho.

Maonesho ya 55 ya Kimataifa ya Vitabu ya Cairo yanaendelea katika mji mkuu wa Misri kwa kushirikisha wachapishaji 1,200 kutoka Misri na nchi zaidi ya 70.

3486971

captcha