IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Jamii yaonyesha mshikamano baada ya kituo cha Kiislamu Cambridge Kanada kupokea vitisho

21:06 - February 16, 2024
Habari ID: 3478362
IQNA - Kituo cha Kiislamu cha Cambridge nchini Kanada kimeungwa mkono na jamii na viongozi wa kisiasa baada ya kupatikana kwa maandishi yenye motisha ya chuki kwenye kuta za jengo lake siku ya Jumatatu.

Mwenyekiti wa kituo hicho, Mohammad Darr, alisema anashukuru kwa mshikamano huo na kwamba hilo ni tukio la kwanza la aina yake tangu miaka ya 1980, Habari za CBC ziliripoti Alhamisi.

Polisi wa Mkoa wa Waterloo walisema walikuwa wakichunguza maandishi hayo yaliyojumuisha msalaba na alama nyingine kama uhalifu wa chuki.

Graffiti hiyo iliaminika kuwekwa kwenye jengo hilo kati ya Jumapili usiku na Jumatatu alasiri.

Waziri Mkuu wa Kanada Justin Trudeau na Kiongozi wa NDP Jagmeet Singh wote walishutumu maandishi hayo ya chuku yaliyoandikwa kwenye kuta cha kitu­­o hicho cha Kiislamu. Katika ujumbe kwenye X, zamani Twitter, Jumatano Trudeau alitaja tukuo hilo kuwa  "la kutisha, la kuchukiza, na lisilokubalika" na Singh alisema linaonyesha kuongezeka kwa chuki dhidi ya Uislamu katika kiwango cha kusikitisha.

Meya wa Cambridge Jan Liggett pia alitoa taarifa, alilaani tukio hilo na kusema limelenga "moja ya taasisi zetu za kitamaduni na za kidini zinazothaminiwa sana".

Alisema maandishi hayo ya chuki hayakuonyesha roho ya jamii na kwamba Cambridge ni nyumba ya wote.

3487210

captcha