IQNA

Fikra za Kiislamu

Kategoria za wanadamu katika Qur'ani Tukufu

10:34 - October 29, 2022
Habari ID: 3476002
TEHRAN (IQNA) - Kuna kategoria tofauti za wanadamu katika jamii. Wakati mwingine, utu na tabia ya binadamu ni lengo kuu, na wakati mwingine hali yao ya kijamii na kiuchumi. Hata hivyo, Uislamu unatilia maanani suala maalum kuhusu wanadamu.

Katika sayansi kama vile sosholojia na saikolojia, kuna kategoria tofauti za wanadamu kwani kila moja huzingatia jambo maalum. Kwa mfano, mwanasaikolojia wa Uswizi Carl Gustav Jung anawaweka watu katika makundi mawili ya watulivu wenye kupenda kutafakari na upweke na kundi jingine ni la wenye kupenda san mwingiliano, mazungumzo na harakati nyingi.

Nao Wamaxi wanapanga watu katika makundi matatu mabepari, wamiliki wa ardhi, na watu wa kawaida ambao aghalabu ni wafanyakazi.

Qur'an Tukufu pia inawaweka wanadamu katika aina kategoria tofauti. Kwa mfano, Surah Al-Fatiha inawaweka wanadamu katika makundi matatu; wale ambao wamepewa baraka, wale walio wanaokabiliwa hasira ya Mwenyezi Mungu, na wale ambao wamepotea. “(Mola) Tuongoe njia iliyonyooka.  Njia ya ulio waneemesha, siyo ya walio kasirikiwa, wala walio potea. (Surah Al-Fatiha, aya ya 6-7).

Surah Al-Baqarah inawaweka wanadamu katika makundi matatu ya waumini, makafiri na wanafiki. Katika aya za mwanzo za Sura zimetajwa sifa za waumini: “Ambao huyaamini ya ghaibu na hushika Sala, na hutoa katika tuliyo wapa.” (aya ya 3)

Kundi la pili ni la makafiri, yaani wale wasioamini upweke wa Mwenyezi Mungu, ni maadui wa dini, na wanapinga imani za kidini waziwazi. " Hakika wale walio kufuru ni sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye, hawaamini." (aya ya 6).

 Aya hii inaashiria sifa ya ukaidi kwa watu hawa kwani hawawezi kuelewa ukweli, kukubali maneno sahihi, na kuacha imani zao potofu kwa sababu wametenda dhambi.

Kundi la tatu ni wanafiki. Quran Tukufu inaelezea kundi hili zaidi ya yale mawili ya mwanzo. Neno “nifaq” kwa Kiarabu linarejelea unafiki na maana yake ni kutofautiana kati ya imani ya ndani na kile mtu anachokionyesha. Aya za Qur'ani na Hadith zinawaelezea wanafiki kuwa wabaya zaidi kuliko makafiri kwani wanaonekana kama marafiki mwanzoni lakini kwa hakika ni maadui. Kwa hiyo, hatari yao kwa jamii ya wanadamu ni zaidi ya hatari ya makafiri.

 “Al-Munafiqun” ni jina la Sura ndani ya Quran na makumi ya aya zinazungumzia sifa za wanafiki na hatari ya unafiki.

Kwa mfano, aya mbili za mwanzo za Surah Al-Munafiqun zinasema: “Wanapo kujia wanaafiki husema: Tunashuhudia ya kuwa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anajua kuwa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu anashuhudia ya kuwa hakika wanaafiki ni waongo. Wamevifanya viapo vyao ni kinga, na wao wakajizuia kuifuata Njia ya Mwenyezi Mungu. Hakika ni mabaya kabisa waliyo kuwa wakiyafanya.

3480975

captcha