IQNA

Fikra za Kiislamu

Uislamu unasisitiza kuheshimu haki za majirani

21:04 - October 30, 2022
Habari ID: 3476007
TEHRAN (IQNA) - Kila mtu anapata fursa kujua baadhi ya watu wanaoishi karibu naye na kuwakubali kama majirani. Ingawa watu hawa hawana uwepo wowote katika maisha yetu ya kibinafsi, wana haki fulani ambazo dini inaona ni muhimu kuwaheshimu.

Maisha ya kijamii ya leo hayawezekani bila kufuata kanuni zilizoainishwa kwani ukiukaji wowote huleta matatizo kwa jamii na mahusiano ya kijamii.

Moja ya masuala muhimu ya kijamii ni yale yanayohusiana na majirani. Jinsi watu wanavyowatendea majirani hutofautiana kutoka kwa tamaduni hadi tamaduni, lakini jambo kuu ni kuheshimu kanuni na maadili.

Kwa mtazamo wa Uislamu, majirani wana nafasi maalum kwani mara nyingi hutajwa kati ya watu wa "karibu". Ndio maana baadhi ya haki zimefafanuliwa kuhusiana na majirani na kuzifuata sio tu kutaleta matokeo chanya hapa duniani bali pia kutaleta thawabu huko Akhera.

Haki za majirani ni muhimu sana hivi kwamba Qur’ani Tukufu na viongozi wa kidini wametoa mapendekezo mbalimbali kuhusiana na jambo hili. Kwa mfano, Qur'ani Tukufu inaelekeza kwenye hitaji la kuwaheshimu majirani kama tunavyosoma: "  Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili na jamaa na mayatima na masikini na jirani wa karibu na jirani wa mbali, na rafiki wa ubavuni na mpita njia, na walio milikiwa na mikono yenu ya kulia. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kiburi wanao jifakhiri, (Surah An-Nisa, aya ya 36)

Ama katika Hadithi ya Mtume Muhammad (SAW), kumuheshimu jirani kumeelezwa kuwa ni sawa na kumheshimu mama yake. "Heshima ya iliyo wajibu kwa jirani ni kama heshima kwa mama wa mtu." (Bihar al-Anwar, v. 76, uk. 154)

Kila mtu anatakiwa kufahamu hali ya jirani yake na kusimama naye katika nyakati ngumu. Akizungumzia haki za majirani, Mtume Muhammad (SAW) alizitaja baadhi ya haki hizo kuwa ni kuwasaidia wakiombwa, kuwakopesha pesa wakiombwa, kuwatimizia mahitaji yao, kuwapa pole wanapopata hasara au matatizo, kuwapongeza kwa matukio ya furaha. (Nahj al-Fasaha, uk. 291)

Katika Hadith nyingine, Mtukufu Mtume (SAW) anataja haki nyingine; kuwapa kikapu cha matunda unapojinunulia na ikiwa hutaki kufanya hivyo, ficha ili majirani wasijutie kutokua na chakula chako na matunda yako, wape sahani ya chakula unapopika chakula kitamu  chenye harufu nzuri. (Kitab al-Kafi, v. 2, uk. 666)

Jambo lingine ambalo limejadiliwa ni ukubwa wa kijiografia wa majirani wa mtu. Imam Sadiq (AS) anasema nyumba arobaini kutoka kila upande zinachukuliwa kuwa majirani.

captcha