IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Matukio 220 ya Kupinga Uislamu yameripotiwa Maryland, Marekani tangu Oktoba 9

22:08 - December 16, 2023
Habari ID: 3478043
IQNA - Takriban malalamiko 220 ya matukio ya chuki dhidi ya Waislamu yamepokelewa na taasisi ya kuwatetea Waislamu katika jimbo la Maryland nchini Marekani tangu Oktoba 9.

Ofisi ya Maryland ya Baraza la Mahusiano ya Kiislamu ya Marekani (CAIR) ilipokea ripoti hizo.

Ofisi hiyo ilitoa ripoti yake ya chuki dhidi ya Uislamu mnamo Ijumaa, Desemba 15.

Ilisema asilimia 32 ya matukio dhidi ya Uislamu yalitokea shuleni na asilimia 13 kati yao yanahusiana na sehemu za kazi.

Tukio hili linakuja wakati Waislamu, Waarabu, na Wapalestina kote Marekani wakiripoti kuongezeka kwa chuki dhidi ya Waislamu na Waarabu tangu Israel ilipoanzisha vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina kwenye Ukanda wa Gaza.

Hivi majuzi, CAIR ilitoa data mpya inayoonyesha kuongezeka kwa malalamiko kwa 216%, ikiwa ni pamoja na matukio ya upendeleo, yaliyoripotiwa katika ofisi zake tangu kuanza kwa vita vya Gaza mnamo Oktoba 7.

Habari zinazohusiana
captcha