IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu Marekani

Waislamu Marekani wataka uchunguzi baada ya Msikiti kuhujumiwa California

21:28 - January 05, 2023
Habari ID: 3476361
TEHRAN (IQNA) –Mhalifu anayeaminika kuwa mwenye chuki dhidi ya Uislamu amehujumu Kituo cha Kiislamu cha Tracy na Msikiti wa Tracy katika jimbo la California la Marekani mkesha wa mwaka mpya.

Tukio hilo lilinaswa kwenye video ya usalama ambayo  inaonyesha mshukiwa akirusha jiwe kubwa kupitia dirisha moja la msikiti huo.

Basim Elkarra, mkurugenzi mtendaji wa Ofisi ya Sacramento Valley/California ya Kati ya Baraza la Mahusiano ya Kiislamu ya Marekani (CAIR-SV/CC), amezitaka mamlaka kuchunguza tukio hilo kama uhalifu unaowezekana wa chuki.

"Kwa sababu nyumba ya ibada ililengwa na kitendo hiki cha uharibifu, tunaziomba mamlaka za kutekeleza sheria kuchunguza sababu ya tukio hili la kutatanisha, kufanya uchunguzi wa haraka na wa kina na kumshtaki mshukiwa pindi atakapokamatwa," Elkarra. alisema katika taarifa. "Licha ya aina hizi za mashambulizi, tutafanya kazi kuunda maeneo salama kwa Waislamu na jumuiya nyingine zote za kidini."

Mwezi Septemba, msikiti mmoja kusini mwa Minneapolis ulipata hasara ya zaidi ya $50,000 baada ya tukio la wizi na uharibifu.

Mnamo Oktoba, makaburi ya Waislamu huko Dakota Kaskazini yalihujumiwa na watu wasiojulikana ambapo viongozi wanaamini tukio hilo lilikuwa "uhalifu wa chuki uliopangwa kabla."

CAIR inawataka Waislamu wa Marekani na taasisi za Kiislamu kuchukua tahadhari zaidi za usalama.

Shirika hilo lilichapisha kijitabu kiitwacho "Desturi Bora kwa Msikiti na Usalama wa Jamii," ambacho kinaelezea hatari inayokabili jamii ya Kiislamu, pamoja na masuluhisho yanayopatikana kwao.

3481958

Habari zinazohusiana
captcha