IQNA

Ubaguzi Marekani

CAIR: Waislamu wa Marekani wanapinga ubaguzi wa rangi

14:05 - September 02, 2022
Habari ID: 3475721
TEHRAN (IQNA) - Baraza la Mahusiano ya Kiislamu ya Marekani (CAIR) lilisema Waislamu wa Marekani wanaunga mkono wale wote wanaopinga ubaguzi wa rangi unaolenga watu wenye asili ya Afrika, chuki dhidi ya wageni, chuki dhidi Uislamu na itikadi kuwa wazungu ndio watu bora zaidi.

Tawi la Michigan la CAIR (CAIR-MI), limetoa wito kwa vyombo vya sheria kumfungulia mashitaka mwanaume mzungu kwa kutoa vitisho vya kikabila baada ya kumshambulia Mwafrika- Mmarekani Dereva wa FedEx wa Marekani huko Portage, Michigan.

Jumamosi Agosti 27, dereva wa FedEx mwenye asili ya Kiafrika ambaye pia ni askari wa akiba wa kikosi cha baharini cha Marekani aliripotiwa kufuatwa, kushambuliwa na kutukanwa na mwanamume mzungu kutokana na rangi yake Portage. Shambulio hilo lililodaiwa kunaswa na kamera ya video, pia lilijumuisha mshukiwa akimfuata mwathiriwa wakati akifikisha kifurushi huku pia akiiba mali ya watu wengine kutoka kwa lori la FedEx. Jina la mshukiwa bado halijatolewa.

"Tunatoa wito kwa vyombo vya sheria kumfungulia mashtaka mshukiwa wa shambulio hili dhahiri, ikiwa ni pamoja na kuzingatia shtaka la vitisho vya kikabila," alisema Mkurugenzi Mtendaji wa CAIR-MI Dawud Walid. "Hakuna mtu anayepaswa kuogopa kutekeleza majukumu yake kutokana na vitisho vya vurugu na chuki za rangi."

Walid pia alitaja kuwa sheria ya jimbo la Michigan ina Sheria ya Vitisho vya Kikabila ambayo ilipitishwa kuwashtaki watu wanaofanya vitendo kama vile katika kesi hii na vile vile kuwa kizuizi kwa watu wanaotaka kuwapiga risasi watu wa rangi.

Alisema CAIR na jumuiya ya Waislamu wa Marekani wanasimama katika mshikamano na wale wote wanaopinga ubaguzi wa rangi dhidi ya Weusi, chuki dhidi ya wageni, chuki ya Uislamu na ukuu wa wazungu.

Dhamira ya CAIR ni kulinda haki za kiraia, kuongeza uelewa wa Uislamu, kuendeleza haki, na kuwawezesha Waislamu wa Marekani.

Habari zinazohusiana
Kishikizo: waislamu cair marekani
captcha