IQNA

Waislamu Marekani

Idadi ya kubwa Waislamu Marekani washinda katika uchaguzi wa Katikati ya Muhula

21:17 - November 11, 2022
Habari ID: 3476073
TEHRAN (IQNA) – Kulingana na ripoti, wagombea Waislamu wa Marekani wamepata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa katikati ya muhula Jumanne uliofanyika katika ngazi za bunge la kitaifa, majimbo na mitaa.

Kumekuwa na rekodi ya idadi kubwa ya ushindi wa wagombea Waislamu wa Marekani katika uchaguzi wa katikati ya muhula wa wiki hii, ripoti ya Jetpac Resource Center na Baraza la Mahusiano ya Kiislamu na Marekani (CAIR) imebaini.

"Nimetiwa moyo na ushindi wa kihistoria tunaouona katika chaguzi za mitaa na majimbo kote nchini. Inaonyesha kuwa jumuiya ya Waislamu inajenga miundombinu imara kwa ajili ya mafanikio endelevu ya uchaguzi," mkurugenzi mtendaji wa Jetpac Resource Centre Mohammed Missouri alisema.

"Maamuzi ya sera kuhusu elimu, makazi, hali ya hewa, na haki za kiraia yanaundwa na mabunge ya majimbo na ni muhimu kwamba sauti yetu iwakilishwe katika mchakato wa kutunga sera."

Abdelnasser Rashid na Nabeela Syed wameshinda uchaguzi wa bunge la jimbo ili kuwakilisha Wilaya za 21 na 51, mtawalia. Wamekuwa Waislamu wa kwanza kuchaguliwa katika Bunge la Jimbo la Illinois.

Nabilah Islam mwenye umri wa miaka 23 amepata ushindi na atawakilisha Jimbo la Wilaya 7 katika Baraza la Seneti la Georgia. Mwanamke huyo mwenye asili ya India ameweka rekodi kama mbunge mwenye umri wa chini zaidi katika baraza hilo la seneti la jimbo la Illinois. Kwa upande wa Baraza la Wawakilishi la Jimbo Georgia, Ruwa Romman amepata ushindi na atawakilisha Wilaya 97.

Munira Abdullahi hakuwa na mpinzani katika uchaguzi mkuu wa  Wilaya ya 9 ya Jimbo la Ohio, na amekuwa Mwislamu wa kwanza kuchaguliwa katika Baraza la Wawakilishi la Jimbo la Ohio. Ismail Mohammad, aliyegombea Wilaya ya 3 katika jimbo hilo Ohio naye pia amepata ushindi na hivyo kuwa mjumbe katika Baraza la Wawakilishi.

Kwa upande wake Mana Abdi aliandika historia alipochaguliwa kuwakilisha  Wilaya ya 95 katika Jimbe la  Maine. Meya wa Portland Kusini Deqa Dhalac ameshinda  katika uchaguzi wa Wilaya ya 120, na hivyo atajiunga na Abdi katika Baraza la Wawakilishi la Maine. Wawili hao wana asili ya Somalia.

Aliyekuwa Diwani wa Jiji la Euless Salman Bhojani, aliyegombea kiti cha Wilaya ya 92 ya Jimbo la Texas amepata ushindi na kuwa Mwislamu wa kwanza kuchaguliwa katika Baraza la Wawakilishi  Jimbo la Texas na hivyo amejiunga na Suleman Lalani, ambaye ambaye amechaguliwa  kuwakilisha Wilaya ya 76.

Uchaguzi huu wa katikati ya muhula ulikuwa na wagombea Waislamu 145 waliogombea ofisi za mitaa, jimbo na shirikisho katika uchaguzi mkuu, wakiwemo wagombea ubunge wa majimbo 48 walioshiriki katika majimbo 23. 

Kwa ujumla  wakati Waislamu 21 wakiwemo Mwanasheria Mkuu wa Minnesota Keith Ellison, Ilhan Omar, Rashida Tlaib na Andre Carson wakichaguliwa tena katika Bunge la Kitaifa la Kongresi, Waislamu wengi wanaungana nao kufikisha idadi ya wabunge Waislamu wa majimbo kote Marekani kufikia 83.

Yamkini idadi ya Waislamu waliochaguliwa katika uchaguzi wa hivi karibuni Marekani ikawa kubwa zaidi kwani kuna wengine ambao hawakutangaza imani yao.

"Msururu wa kihistoria wa ushindi wa Waislamu wa Marekani uliovunja rekodi ni uthibitisho wa kuongezeka kwa jumuiya yetu katika siasa za Marekani na nukta hii inaashiria kuwa majirani zetu wana imani nasi kuwawakilisha na kupigania maslahi yao," mkurugenzi mkuu wa taifa wa CAIR Nihad Awad alisema.

"Tunashuhudia hatua inayofuata katika mageuzi ya kisiasa ya jumuiya ya Waislamu wa Marekani kutoka kwa sauti zilizotengwa ambazo ziliwekwa kando, hadi kuwa watoa maamuzi. Maafisa hawa wapya waliochaguliwa wanajenga juu ya mafanikio ya uwekezaji wa miongo kadhaa ya jumuiya yetu katika ushiriki wa raia, wapiga kura kujiandikisha na kugombea nafasi hizo."

3481200

captcha