IQNA

Uislamu Marekani

Elon Musk atakiwa ajifunze kuhusu Uislamu baada ya Tweet yenye utata

15:53 - January 02, 2023
Habari ID: 3476345
TEHRAN (IQNA)- Bilionea wa Kimarekani, Elon Musk, ambaye ni mmiliki wa mtandao wa kijamii wa Twitter, amewakasirisha Waislamu nchini Marekani baada ya kuchapisha picha kwenye akaunti yake ya Twitter, ikiwa na idadi ya alama za fikra na itikadi anazodai zinalenga "kupindua na kuharibu fikra na akili za watu."

Picha iliyowekwa na Elon Musk kwenye ukurasa wake wa Twitter ikiandamana na maneno: "Mimi sijapinduliwa akili", ina rangi za bendera za mashoga, nyota inayoashiria itikadi ya kikomunisti, pamoja na mwezi mpevu, ambao Musk ameuweka hapo kama kiashiria cha dini ya Uislamu.

Mara tu baada ya kuchapishwa twitter hiyo yenye utata, Baraza la Mahusiano ya Kiislam na Marekani (CAIR) limetangaza upinzani wake mkubwa dhidi ya maudhui ya ujumbe huo wa Musk na kuutaja kuwa ni "hujuma na kueneza chuki dhidi ya Uislamu."

Baraza la Waislamu la Marekani limejibu ujumbe wa Musk, na kuandika kwenye Twitter kwamba: "Elon Musk, tunaweza kukubali utani, lakini Uislamu sio sawa na ukomunisti, na haulengi kupindua na kupotosha akili za watu."

CAIR pia imemtaka Elon Musk ajifunza zaidi kuhusu Waislamu na Uislamu, "ambayo imesema, unaweza kumpa amani katika maisha haya ya dunia na baadaye, ambayo haiwezi kununuliwa kwa pesa na umaarufu!"

Tangu kuanzishwa kwake mwaka wa 1994, CAIR imekuwa shirika kubwa zaidi la kutetea haki za Waislamu nchini Marekani, na baraza hilo lina ofisi na matawi 31 ya kikanda.

Baraza hilo la Waislamu wa Marekani linalenga kupanua uelewa wa Uislamu, kuhimiza mazungumzo, kulinda uhuru wa raia, kuwatetea Waislamu wa Marekani, na kujenga miungano inayokuza haki na maelewano.

3481900

Habari zinazohusiana
captcha