IQNA

Hali ya Palestina

Vita na mateso Gaza wakati wa kukaribia Ramadhani

20:35 - March 08, 2024
Habari ID: 3478469
IQNA - Mashambulio yasiyokoma ya utawala katili wa Israel kwenye Ukanda wa Gaza uliozingirwa yamewanyima Waislamu duniani furaha ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kwa Waislamu ulimwenguni kote, Ramadhani ni wakati wa sala, tafakari na furaha wakati wa milo ya jioni ya futari, lakini watu wote wa Gaza wanatamani mwaka huu Ramadhani iwe mwisho wa miezi mitano ya vita na mateso.

Ni matumaini ya pamoja kote katika ulimwengu wa Kiislamu, ambapo mawazo ya wengi yako Gaza kabla ya mfungo wa mwezi mwezi mtukufu wa Ramadhani unaotazamiwa kuanza Jumatatu au Jumanne kwa kutegemea mwezi mwandamo.

Katikati ya magofu ya kusini mwa Gaza, Nevin al-Siksek aliketi hivi majuzi nje ya hema lake la muda, akiwa na binti yake mdogo akijaribu kumfanya asahau  mauaji yaliyowazunguka kwa kuwasha taa ya plastiki ya Ramadhani.

Taa ya jadi ya Ramadhani ambayo ni maarufu kama  "fanous"ni ishara mahususi ya mwezi wa tisa wa kalenda ya Kiislamu, mwezi ambao Waislamu hufunga kula na kunywa an kujuzuia na mambo mengine yote waliyokatazwa katika mchana wa mwezi huu kuanzia alfajiri hadi jioni. Nyakati bora zaidi kwa familia na marafiki katika mwezi huu ni ule mjumuiko wa milo ya jioni ya iftar.

Katika Gaza mwaka huu, taa hizo ni miongoni mwa ishara chache zinazoashiria mwezi mtukufu unaokuja, huku kukiwa na onyo kali la njaa kubwa.

Wakati wapatanishi wa kimataifa walikuwa na matumaini ya kusitishwa vita kwa wakati kwa ajili ya Ramadhani, hakuna mafanikio yoyote yaliyokuja kufikia Ijumaa.

Sehemu kubwa ya eneo la watu milioni 2.4 imekuwa taswira ya kijahanamu ya vitongoji vilivyolipuliwa na mabomu, watoto waliodhoofika na makaburi ya halaiki.

Vita vya Gaza vilizuka baada ya Harakati ya Kiislamu ya Kupigania Ukombozi wa Palestina, Hamas, kufanya operesheni isiyo na kifani dhidi ya eneo linaloikalia kwa mabavu tarehe 7 Oktoba ambayo ilikuja kujibu ongezeko la ukatili wa utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina.

Kampeni ya kijeshi ya utawala dhalimu wa Israel iliyoanza baada ya operesheni hiyo ya kujitetea ya Wapalestina imesababisha vifo vya takriban watu 30,800 hadi sasa, idadi kubwa ya wanawake na watoto.

Sehemu nyingine za ulimwengu wa Kiislamu zinaweza kuwa zinapambana na changamoto zao, kuanzia  migogoro ya kisiasa, kijamii, na mapigano hadi mfumuko mkubwa wa bei. Lakini Waislamu wengi wanasema mawazo yao yako kwa Wapalestina mwaka huu huku kukiwa na ripoti za njaa inayonyesha huko Gaza, ambapo wakaazi waliokata tamaa wamekula farasi waliochinjwa na hata majani ambayo kawaida hayatumiki kama chakula. Taarifa zinasema Wapalestina wengi, hasa watoto wamekufa njaa. Ni wazi kuwa utawala haramu wa Israel sasa unatumia njaa kama silaha ya vita baada ya kushindwa katika mapigano ya silaha.

Kwingineko, Waislamu katika al-Quds (Jerusalem) inayokaliwa kwa mabavu wana wasiwasi kuhusu ghasia katika eneo la msikiti wa Al-Aqsa. Wakati wa Ramadhani, Waislamu kwa makumi na hata mamia ya maelfu husali katika msikiti huu ambao ni eneo la tatu kwa utukufu katika Uislamu.

Lakini mwezi Februari, waziri mwenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia wa Israel Itamar Ben Gvir alisema kuwa wakaazi wa Palestina wa Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu "hawapaswi kuruhusiwa" kuingia al-Quds wakati wa Ramadhani.

Ofisi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ilisema Jumanne kwamba waumini wataruhusiwa kuingia msikitini "kwa idadi sawa" na miaka iliyopita.

3487471

Habari zinazohusiana
captcha