IQNA

Umoja wa Waislamu

Israel imewaua Wapalestina Gaza kutokana na ukosefu wa umoja wa Waislamu duniani

15:56 - November 28, 2023
Habari ID: 3477956
TEHRAN (IQNA) – Mauaji ya kimbari ambayo yanatekelezwa na utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina huko Gaza yalitokea kwa sababu Umma wa Kiislamu umegawanyika, jambo ambalo ni la kusikitisha kabisa, mchambuzi wa masuala ya kisiasa na umma wa Nigeria amesema.

"Kwa umoja wa Uislamu, mauaji ya halaiki huko Gaza yangeweza kuepukika na kuzuilika," Harun Elbinawi aliandika katika makala liyochapishwa na Press TV ifuatavyo:

Katika wiki kadhaa zilizopita, tumeshuhudia mauaji ya kikatili yakitokea katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa. Utawala wa Israel ambao unaua watoto kiholele umetekeleza msururu wa mauaji, kwa kushambulia kwa mabomu popote pale ulipotaka katika Ukanda wa Gaza.

Jeshi katili la Israel limekuwa likiua watu majumbani mwao, hospitalini, sokoni, misikitini na makanisani. Mauaji hayo ya kimbari dhidi ya Palestina yametekelezwa bila huruma kutokana na usambazaji mkubwa wa silaha za Marekani.

Utawala huo katili umeangamiza kabisa mamia ya familia za Wapalestina tangu Oktoba 7. Watoto wachanga wameuawa wakiwa katika inkubeta hospitalini na wazee wameuawa wakiwa usingizini.

Hadi sasa idadi ya waliouawa katika hujuma ya Israel tayari  imevuka 15,000 huko Gaza, wengi wao wakiwa watoto na wanawake wasio na hatia. Na kuna zaidi ya watu 2,000 waliofukiwa kwenye vifusi.

Licha ya mapatano hayo ya siku nne ya usitishaji , ambapo pia pande mbili zimebadilishana wafungwa na mateka, kumekuwa na ripoti kuhusu ndege za kivita za utawala wa Israel kuendelea kushambulia Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Idadi ya misikiti iliyoharibiwa kabisa imehesabiwa kuwa 85, na iliyoharibiwa kwa kiasi inaripotiwa kuwa 174, pamoja na angalau makanisa matatu ambayo yameharibiwa kwa kiasi au kabisa.

Ukiungwa mkono na madola ya Magharibi, utawala ghasibu wa Israel umefanya mauaji ya kutisha dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza katika kipindi cha wiki saba zilizopita, yakiwemo katika kambi finyu za wakimbizi.

Idadi ya majeruhi imezidi 35,000 huku zaidi ya asilimia 75 kati yao wakiwa ni watoto na wanawake, kwa mujibu wa mamlaka ya afya ya Palestina na makundi ya misaada huko Gaza.

Hebu tuelekee moja kwa moja kwenye jambo hili: Mauaji ya halaiki huko Gaza yalitokea kwa sababu Umma wa Kiislamu umegawanyika, jambo ambalo ni la kusikitisha kabisa.

Iwapo kungekuwa na umoja halisi baina ya Waislamu duniani kote, mauaji ya halaiki huko Gaza yangeweza kuepukika na kuzuilika. Mgawanyiko huleta udhaifu. Ikiwa umegawanyika, utafanywa dhaifu. Umoja ni nguvu.

Waislamu wasisahau ukweli kwamba mkakati wa "kugawanya ili kutawala" wa madole ya kibeberu ya Magharibi umeundwa dhidi yao. Mgawanyiko kati ya Waislamu unanufaisha madola hayo ya kibeberu.

Wamagharibi daima wamekuwa na nia ya kuchochea mgawanyiko baina ya Waislamu wa madhehebu za Sunni dhidi ya Shia, jambo ambalo hurahisisha kwao kutekeleza malengo yao ya kugawanya na maovu.

Nilizaliwa Sunni na kwa muda wa miaka 30 sasa nafuata madhehebu ya  Shia. Kwa unyenyekevu wote, nasema, kama mwanafunzi,  nimeweza kufanya utafiti kuhusu madhehebu za Shia na Sunni. Nathubutu kusema hakuna tofauti kubwa kati madhehebu hizi.

Kwa bahati mbaya, adui mbaya na mbaya ameweza kukuza tofauti ndogo kati ya jamii hizi mbili kwa msaada wa baadhi ya falme za Kiarabu na kutumia migawanyiko hii kwa maslahi yake.

Kwa adui, ni sawa na kumuua Mpalestina wa madhehebu ya Sunni  na Mlebanon wa madhehebu ya Shia. Hatofuatishi baina yao. Vita adui ni dhidi ya Waislamu na dhidi ya matukufu ya Uislamu, ukiwemo Msikiti mtukufu wa Al-Aqsa.

Palestina ni nembo umoja wa Waislamu. Matukio yanayoendelea katika Ukanda wa Gaza yanapaswa kuwa kama mwito wa kuamsha mataifa ya Kiislamu kuungana kwa lengo kubwa zaidi.

Ni lazima tujiulize: Je, mgawanyiko huu ni faida au hasara kwa Waislamu? Je, ni akina nani wanaofaidika na mifarakano ya Waislamu? Na kinyume chake, ni akina nani wanaonufaika na umoja wa Waislamu?

Madola ya kibeberu ya Magharibi na utawala wa Kizayuni wa Israe ndio wanufaika wakubwa wa mfarakano na migawanyiko baina ya Waislamu.

3486191

Habari zinazohusiana
captcha