IQNA

Kadhia ya Palestina

Wapigania ukombozi Palestina wahimiza Kampeni ya Kimataifa ya ‘Kimbunga cha Ramadhani’

17:49 - March 04, 2024
Habari ID: 3478449
IQNA - Makundi kadhaa ya wapigania ukombozi wa Palestina yametoa wito kwa watetezi wa haki kote ulimwenguni kujiunga na kampeni ya kimataifa iliyopewa jina la "Kimbunga cha Ramadhani.

Kampeni hiyo inajumuisha maandamano katika sehemu mbalimbali za dunia wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa mshikamano na Gaza na Palestina.

Utawala wa Israel ulianzisha vita vya mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza mnamo Oktoba 7 na hadi sasa vita hivyo vya mauaji ya kimbari vimepelekea kuuawa Wapalestina wasiopungua 30,410, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na wengine 71,700 kujeruhiwa.

Pia kumetokea uharibifu mkubwa, huku karibu wakazi wote karibu milioni mbili wa Gaza wakilazimika  kuyahama makazi yao. Aidha njaa imeenea kote katika eneo hilo kutokana na vita na mzingiro wa utawala wa Israel.

Katika taarifa siku ya Jumapili, makundi ya Wapalestina yalitoa wito kwa watu kushiriki katika kampeni ya ‘Kimbunga cha Ramadhani' katika ngazi ya kitaifa, kikanda na kimataifa.

Wamesisitiza haja ya kuungwa mkono suala la Palestina na mashinikizo kwa utawala wa Kizayuni usitishe vita vyake vya mauaji ya kimbari dhidi ya Ghaza.

Pia walitoa wito wa kupanua mgomo dhidi ya Israel kwa njia mbalimbali.

Makundi hayo yamesisitiza haki ya watu wa Palestina ya uhuru na kujitawala pamoja na haki yao ya kurejea katika nchi yao na kuanzisha nchi huru na mji mtakatifu wa al-Quds ukiwa mji mkuu wake.

Taarifa hiyo imelaani zaidi utawala wa Kizayuni wa Kizayuni wa Israel kwa kuendelea kujenga vitongoji haramu na uvamizi wa mara kwa mara katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, na pia sera ya utawala huo wa Kizayuni ya kuhujumu al-Quds (Jerusalem) na kuvunjiwa heshima matukufu ya Kiislamu na Kikristo katika mji huo mtakatifu.

4203353

Habari zinazohusiana
captcha